EAEP Kiswahili Angaza Akili Pevu Grade 5 | Text Books

 EAEP Kiswahili Angaza Akili Pevu Grade 5 Available

EAEP Kiswahili Angaza Akili Pevu Grade 5

Availability: yes
Ksh.0.00 Ksh.515.00
+
Buy Now
Sold By     GoBooks Delivery
Successful Sales: 1,000 items
Delivery: 1-3 Days Pay on delivery
Category: Kiswahili
Education Level: Lower Primary
Age Group: Grade 5
Requisition: Recommended
Author: S. Otieno, M. Banda
Publisher: East African Educational Publishers

Quick Overview

Kiswahili Angaza, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 5 ni kitabu kilichosukwa na kuwambwa kwa makini na kwa kina kirefu. Kitabu hiki kimetosheleza mahitaji ya mtalaa wa umilisi. Kinakuza umilisi uliopendekezwa kwenye mtalaa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo unaomwegemea mwanafunzi zaidi na kumfanya mwalimu awe mwelekezi tu wala si mtoaji wa elimu. Kitabu hiki kitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia kwa stadi za kusikiliza na kuzungumza, Kusoma, Kuandika na Sarufi. Kitabu hiki kimezingatia: • Lugha nyepesi iliyokomaa na inayoweza kueleweka na mwanafunzi kwa urahisi. • Mada zilizopangwa kwa kuzingatia mtalaa. Kila mada inaanza kwa picha ambazo zimechorwa vizuri na kikamilifu. Picha hizi zitasisimua hali ya mwanafunzi ya kujifunza. • Shughuli mbalimbali ambazo zinawashirikisha wanafunzi wakiwa peke yao, wawili wawili au katika vikundi. Shughuli hizi zinakuza stadi nyingi za kufikiria kama vile kuchanganua, kutambua, kubainisha na kuhakiki. • Ushirikisho wa wazazi na walezi ambao unaimarisha uwajibikaji wa wanafunzi. Waandishi wa kitabu hiki wana uzoefu mwingi na wamekiandika kitabu hiki kwa utaalamu mkuu. ISBN: 9789966564610